Je, Ndoa yako..Ina Matatizo?....Ingia hapa


MCHUMBA WANGU NILIMPATA KANISANI…. LAKINI MACHO YANGU YALINIDANGANYA!!!>>>>

Pasaka hii ilikua mbaya sana kwangu maana sikuwa na furaha ila machungu mara mbili. Kwanza kwa kufiwa na msanii wetu lakini kikubwa zaidi huu ndio wakati nilipothibitishiwa kuwa mpenzi wangu ambaye nilitarajia kumuoa…Anasaliti penzi langu..
Ilikua Jumamosi ya pasaka ambapo nilipata ugeni nyumbani.mgeni mwenyewe ni huyu mchumba wangu ambaye katka wiki iliyotangulia nilipata hisia kuwa ananisaliti hivyo tukahitilafiana nikaamua kuwa mbali naye kwa muda ili kutafuta ukweli kwa vyanzo vingine maana sasa naamini kuwa lisemwalo lipo…kama halipo laja.
Siku hii alipokuja alikuwa na lengo la kujaribu kunilainisha nibadili msimamo wangu na kuondoa mawazo nilokuwa nayo juu yake….mambo yakawa tofauti sana wala sikutarajia kusikia yale nilosikia!!!!!
Nilijiuliza mambo mengi sana …Ni huyu ambaye nilimuona kwa mara ya kwanza kanisani nikampenda???????...Ni huyu ambaye ni mkimya muda wote ambaye hata sura yake ni ya upoleee??????
Iliniuma sana sana sana sana hata siwezi kuelezea baada ya kusikia hayo nilosikia…..Mmmh! We acha tuu inaumaaaaa!
Kwa sasa nimemwacha aendelee na hao watu wate ila kwa kweli inaniuma mno na wala siwezi kueleze….Lazima niseme kweli ninaumia mnoooo siwezi kusema…

Najua Bado Nampenda sana kutoka ndani lakini Moyo Wangu unakataa kabisa kuamini kuwa naweza kumuoa mwanake wa namna hii……
Tafadhali nishauri nifanyeje!!????

3 comments:

  1. Wadau mchango wenu unahitajika katika hili....

    ReplyDelete
  2. Dah...Aisee nakuonea huruma sana kaka yangu...Lakini ndo ujue sio kila king'aacho ni dhahabu, vingine ni rangi yake tuu. huyo dada kwa vyovyote vile sio mwaminifu hata akifanywaje! Yaani kama ni samaki sio aliyechina bali aliyeoza, maana hata ndimu haiwezi kukata harufu yake mbaya na wala hawi mtamu hata chembe..Mie nakushauri wewe achana nae kabisaa, vinginevyo utajuta sana huko mbele..

    ReplyDelete
  3. inaonesha inahuzunisha lakini umeiminya sana story yenyewe. mimi naomba kama ungeitoa yoote kabisa ili tuweze kujua tunakushauri vipi. Wewe tushirikishe yoote kabisa ili tujue la kusema kwa uwazi zaidi.

    ReplyDelete